KIFO CHA ISMAIL KHALFAN MRISHOKIFO CHA ISMAIL KHALFAN MRISHO
Mchezaji chipukizi, Ismail Khalfan Mrisho (19), alianguka na kufariki dunia wakati akiitumikia timu yake kwenye ligi ya vijana chini ya miaka 20.
Akivaa jezi namba 4, Ismail alifunga bao la kwanza dakia 30( la 4 kwake kwenye mashindano) na kushangilia kwa mtindo wa kinyoka nyoka.
Takribani nusu saa baadaye, aliangushwa kimchezo lakini hakiunuka tena. Jitihada za kuokoa maisha yake zilifanyika lakini haikuwa bahati na akapoteza maisha.
Inasemekana kwamba miezi kadhaa iliyopita, alipata mwaliko nchini Marekani kushiriki mashindano ya vijana na aliibuka mfungaji bora